Kutokana na kupungua huko, inamaanisha kwamba simu feki nchini zinazidi kupungua.
Akizungumza na vyombo vya habari leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA James Kiraba amesema katika uchambuzi na matokeo ya awali ambacho pia kilishirikisha kampuni za mawasiliano kimeonyesha kuwa mwezi Februari ilishuka mpaka asilimia 18.
Amesema uchambuzi wa Februari ulionyesha idadi ya namba tambulishi ambazo hazikuwa na viwango zilikuwa asilimia tatu, vilevile idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa na asilimia 18, huku simu halisi zikiwa asilimia 79.
"Uchambuzi wa Machi unaonyesha idadi ya namba tambulishi ambazo hazina viwango zilikuwa sawa na asilimia mme, huku idadi ya namba tambulishi ambazo zimenakiliwa zilikuwa asilimia 13. Uchambuzi huu unahusisha kampuni zote za simu nchini," amesema Kiraba.
0 Response to "Wananchi Wamelielewa Soma la TCRA...Simu Feki Nchini zazidi Kupungua...."
Post a Comment