Mahakama ya Wilaya ya Ilala imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela
mkazi wa Ukonga Mombasa, Christina Yoram (31) baada ya kupatikana na
hatia ya kumjeruhi mtoto wake wa kambo wa kiume wa miaka 11 kwa kumchoma
na pasi.
Mshtakiwa huyo pia alimpiga sehemu mbalimbali za mwili mtoto huyo na kumsababishia majeraha.
Akisoma hukumu hiyo jana Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan alisema
mahakama hiyo imetoa adhabu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi dhidi
yake uliotolewa na mashahidi watano.
“Vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watoto bado ni tatizo katika jamii,
hivyo kutokana na mahakama yangu kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na
upande wa mashtaka, mshtakiwa utatumikia kifungo cha miaka mitatu jela
ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizi,” alisema Hakimu
Hassan.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, Wakili wa Serikali Chesenci Gavyole
aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa huyo ili iwe
fundisho kwa wanawake wengine wenye tabia mbaya kama yake. Kabla ya
hukumu hiyo, mahakama hiyo ilitoa nafasi kwa mshtakiwa huyo kujitetea
ili isimpe adhabu kali.
Katika utetezi wake, aliiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa madai
kuwa ana Ukimwi, watoto watatu na mama yake mzazi wanaomtegemea na
kwamba mume wake amepooza mwili kwa kiharusi.
Awali Wakili Gavyole alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Machi 20, 2013 eneo la Ukonga Mombasa Wilaya ya Ilala
News
Tuesday, May 10, 2016
0 Response to " Jela Miaka Mitatu Kwa Kumchoma na Pasi Mwanaye"
Post a Comment