Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Vincent Mashinji
amesema kitendo cha Serikali ya Awamu ya Tano kuzuia matangazo ya moja
kwa moja ya Bunge ni sawa na kuling’oa meno bunge hilo.
Tofauti na mikutano miwili iliyopita ya Novemba 2015 na Januari/
Februari 2016, Serikali hii inayoongozwa na Rais John Magufuli, iliamua
kufuta matangazo ya moja kwa moja ya Bunge la Bajeti lililoanza vikao
vyake Aprili 19 kwa maelezo kwamba ni gharama kubwa kwa Shirika la
Utangazaji la Taifa (TBC). Badala yake TBC huonyesha kipindi cha maswali
na majibu pekee na hurekodi matangazo mengine na kurushwa katika
kipindi cha ‘Leo katika Bunge’ saa nne usiku.
Suala hilo lilipingwa vikali na wabunge wa upinzani lakini uongozi wa
Bunge ulitia chumvi kwenye kidonda baada ya kukataza vyombo vya habari
kupiga picha za video, badala yake wanatakiwa kuchukua picha kutoka kwa
televisheni ya Bunge.
Akizungumzia hali hiyo jana alipofanya ziara katika ofisi za gazeti hili
zilizopo Tabata jijini Dar es Salaam, Dk Mashinji alisema kuwa huu ni
mkakati maalum uliosukwa na CCM ili kuvibana vyama vya upinzani
News
Tuesday, May 10, 2016
0 Response to "Chadema: Bunge la Sasa Kibogoyo Limeng'olewa Meno na Serikali"
Post a Comment