Wanawake wengi hupata mimba kwa kutojua mzunguko wao. Mwanamke anayejitambua lazima awe na calenda ya miezi sita ya mzunguko wa hedhi yani usihesabu kila mwezi unaanza upya kwani unaweza zikapungua au kuzidi uwe na kalenda ya miezi ya nyuma.
Tunaposema mzunguko wa hedhi anza kuhesabu kuanzia siku uchafu wa yai unapotoka kwa njia ya uke (kutokwa na damu) ambayo huchukua kuanzia siku 1~5
Siku ya 6~ 9 ni siku Kavu (uwezekano wa kutopata mimba) kwanini tunasema uwezekano wa kutokapa mimba kwa sababu siku ya 10 yai linaanza kuzalishwa upya kumbuka mbegu za kiume huishi ndani ya kuta za mwanamke ndani ya siku 2-3 kwa hiyo ukifanya mapenzi ndani ya siku ya 8 au 9 unaweza pata mimba pale ambapo mbegu zikiwa zinaishi bado ndani ya uke.
Siku ya 10-17 ni za HATARI hapo yai huwa lishakuwa tayari na kama ukifanya mapenzi siku hizo mimba kupatikana ni rahisi japo wakati mwingine huwa sio rahisi kwa kutokana uogeleaji wa mbegu za kiume kama hazitakua na nguvu za kwenda kurutibisha yai lilipo kwenye kuta zake.
Siku ya 18-20 hizi tunaziiita ni siku 3 HATARISHI sana kwa sababu yai hutoka kwenye kuta za uzazi na kwenda moja kwa moja mpaka kwenye mfuko wa uzazi kwa ajili ya kusubiri kurutubushwa na mbegu za kiume. Siku hizo tatu endapo ukifanya mapenzi kwa kinga (Kondom) na ikapasuka huwa ni rahisi sana kupata mimba kwa sababu yai huwa karibu kwa hiyo mbegu zitakazotoka hazitoogelea sana zitafikia yai haraka na kulichavyusha. Ndio maana wengi hujiuli "Mbona nimetumia kondomu lakini nimepata mimba" jibu ni kuwa huwenda hukujua siku zako hatarishi sana.
Siku ya 20~31 nakuendelea japo kuna utofauti wa kwendahedhi wengine huwa ni mda mfupi wa siku 21~26, mrefu wa siku 28~35 hii hutokana na hali ya mwili wa muhusika.
Siku hzio tunasema ni KAVU (salama) kwani yai likiishi siku tatu bila kurutubishwa linaanza kuharibika kujiandaa kutoka nje ambayo siku hizo mwanamke maumivu ya tumbo huyasikia sikia mpaka pale siku kamili inapofika hutoka kwa njia ya damu.
USHAURI: Kwa kuangalia siku ambazo ni SALAMA sana ni siku 1 ~ 2 baada ya kumaliza hedhi. Au kama ni muoga na MCHAFU wengine hujikuta wanafanya tendo la ndoa siku ambazo yuko hedhi bila kujua hatari zake.
kwa msaada na mawasiliano zaidi whatsapp 0787325447 au 0673774965,
Imeandaliwa na Dk.Dominick Chuwa (Facebook
0 Response to "TAMBUA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI KWA MWANAMKE (SIKU SALAMA, ZISIZO SALAMA NA SIKU HATARISHI)"
Post a Comment