Kundi la muziki, Navy Kenzo ambalo linaundwa na wasanii wawili, Nahreal
pamoja na Aika, ni moja kati ya makundi machache ya muziki nchini ambayo
yanawekeza pesa nyingi katika kuandaa kazi zao.
Navykenzo
Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Nahreal amesema tayari wameshaanza
kurudisha pesa zao ambazo wamekuwa wakiwekeza kwenye muziki kwa muda
mrefu.
“Gharama ambazo tumetumia ni kubwa na tunajua muziki ni uwekezaji,
lazima uwekeze, kwa hiyo mwanzo tulikuwa tunaweka pesa nyingi lakini
hazikuwa zinarudi, so tumefika wakati pesa imeanza kuingia. Kama tour
yetu imetupatia pesa fulani, pia wimbo wetu ‘Kamatia Chini’ umetupatia
deal kubwa. Kwa hiyo pesa ambayo tuliwekeza inarudi kwa njia nyingi,
makampuni, show, na issue nyingine,” alisema Nahreal.
Pia katika hatua nyingine Nahreal amewataka mashabiki wake kusubiria kazi mpya pamoja na kolabo za kimataifa.
entertaiment
Sunday, May 8, 2016
0 Response to "NAVY KENZO AMESEMA , Pesa Tulizowekeza Kwenye Muziki zimeanza Kurudi.........."
Post a Comment