Bongo ina wasanii wengi sana, kati yao 90% hawajui muziki kifupi ni
wabovu akiwemo Diamond ila wanapendwa kupita maelezo, na 10% wanajua
muziki kifupi ni wakali akiwemo Rama dee na Steve wa RnB ila cha
kushangaza hawapendwi(muziki wao).
Sasa nashindwa kuelewa inakuwaje?? Mfano huyu Diamond miziki yake ni ya
kawaida tu lakini raia wanamshobokea vibaya sana, kila ngoma anayotoa
inakuwa ni national anthem lakini nikisikiliza mi naona ni miziki tu ya
kawaida ambayo hata kwenye flash au laptop au memory card yangu siwezi
kuweka.
Sijajua watu ni kwamba hawajui muziki au ni nini tatizo au ni ufreemason
na uganga wa kupumbaza watu?? Kama ni mganga basi ni kiboko aisee,
nasema ukweli ngoma za jamaa ninazozikubali ni Nitarejea na kesho, basi!
entertaiment
Sunday, May 8, 2016
0 Response to "MH HATA BADO., Sijajua watu Wanaupendea nini Muziki wa Diamond Platnumz"
Post a Comment