
KIWANGO cha pensheni kwa wastaafu walio kwenye mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii waliokuwa wakilipwa kima cha chini Sh 50,115 kinatarajiwa kuongezwa kwa asilimia 100 hadi Sh 100,125.
Naibu Waziri Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema jana bungeni kwamba, wastaafu hao wataanza kulipwa kiwango hicho kipya pamoja na malimbikizo yao baada ya utaratibuunaoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Mifuko hiyo (SSRA) kukamilika
Kijaji alisema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Conchester Rwamlaza (Chadema), aliyetaka kufahamu ni lini wastaafu wataanza kulipwa fedha hizo. Mbunge huyo alisema tangu bajeti inayoisha ya mwaka 2015/16, serikali kupitia wizara ya fedha iliahidi kupandisha pensheni kwa wastaafu wanaolipwa Sh 50,000 ili walipwe 100,000.
0 Response to "KUTOKA BUNGENI:HATIMAE SERIKALI YAPANDISHA PENSHENI KWA 100%"
Post a Comment