Baada ya Kampuni ya UDA-RT kuwasilisha maombi ya nauli zitakazotumika
kwa mabasi yaendayo haraka kwa Mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu
na majini (SUMATRA), leo hii (May 09 2016) SUMATRA imetangaza nauli
hizo.
SUMATRA imesema kuwa njia ya pembezoni (Freeder Route) nauli ya mtu
mzima ni 400 na mwanafunzi 200 na njia kuu (Trunk Route) ni 650 na
mwanafunzi 200 na kwa abiria atakayetumia kusafiri njia kuu (Freeder
Route) na kuendelea na safari kwa njia ya pembezoni nauli yake itakuwa
ni 800 na mwanafunzi 200.
Huduma hiyo itatolewa kuanzia kesho bure kwa wananchi kwa siku mbili
mfululizo na ifikiapo May 12 2016 zitaanza kutozwa nauli zilizotajwa.
Msimamizi wa mradi kutoka DART, Injinia Ronald Lwakatare amesema haya wakati akiongea na waandishi wa habari mchana huu;
‘Wakati huo tunafanya majaribio tutakuwa tunaangalia mfumo unavyofanya
kazi kwa hiyo tutawabeba abiria kwa siku kadhaa bila kulipa nauli’
News
Monday, May 9, 2016
0 Response to " SUMATRA yatangaza nauli kwa mabasi yaendayo kasi"
Post a Comment