Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Singida, Simion Mumbee
amesimamishwa kazi baada ya kudaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu
watumishi hewa.
Katika taarifa hiyo, Mumbee anadai watumishi hewa 19 waliogundulika
kwenye halmashauri hiyo hawajaisababishia hasara Serikali jambo
linalodaiwa kuwa si kweli.
Akizungumza jana kwenye ufunguzi wa kikao cha maendeleo mkoani humo,
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe alisema anamsimamisha kazi
mkurugenzi huyo ili kupisha uchunguzi.
“Nilipotuma tume kufuatilia suala la watumishi hewa katika Halmashauri
ya Wilaya ya Singida, ilibaini wapo na wameisababishia Serikali hasara
ya zaidi ya Sh125 milioni,” alisema Mtigumwe.
Alisema taarifa ya Mumbee ililenga kuidanganya Serikali. Mtigumwe
alimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa, Dk Angela Lutambi kumuandikia barua ya
kumsimamisha kazi mara moja.
Mtigumwe alisema hana nafasi ya kufanya kazi na watumishi wa aina ya Mumbee.
Wakati huo huo; Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amemsimamisha
kazi Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Philbert Mtweve
kwa tuhuma za kuwalipa mishahara watumishi hewa wanane na kuisababishia
Serikali hasara ya Sh27 milioni
News
Friday, May 6, 2016
0 Response to "Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Singida Asimamishwa Kazi Baada ya Kutoa Taarifa za Uongo Kuhusu Watumishi HEWA"
Post a Comment