Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameshauri kufungwa kwa kamera
maalumu za CCTV kwenye nyumba zote za kulala wageni na hoteli ili
kuimarisha ulinzi.
Ushauri huo wa Mwita unakuja baada ya siku sita kupita , kutokea kwa tukio la mwanamke mmoja kufariki dunia akiwa gesti.
Mwita ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), alisema
mamlaka husika wakiwamo wamiliki wa hoteli na nyumba hizo waliangalie
suala hilo kwa jicho la tatu kwani litasaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia
matukio kama hayo.
“Kamera hizi zisifungwe chumbani bali zifungwe maeneo ya nje na
mapokezi kwenye jingo husika.Hii ni njia sahihi ya kupambana na matukio
kama haya maana hili lipo hivi linaweza kutoke lingine zaidi ya hili,”
alisema Mwita ambaye alishika madaraka hayo Machi 22mwaka huu.
Mbali na hilo, Mwita alisahauri pia kuboreshwa kwa mfumo usalama katika
maeneo mbalimbali ili kuzuia vitendo kama hivyo vya kinyama
vinavyokatisha uhai wa binadamu.
Hata hivyo , Mwita aliwaomba viongozi wa dini wa mkoa wa Dar es Salaam,
kuendelea kutoa elimu kwa umma ili wakazi wa jiji hilo kumrudia Mungu
na kuachana na vitendo vya kinyama.
Pia meya huyo amekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya
kijamii zikimnukuu yeye kuwa ameshauri wamiliki wa gesti kuwapiga picha
wageni wanaokwenda kulala kwenye nyumba hizo.
Hivi karibuni mwanamke huyo jina limehifadhiwa alikutwa amefariki dunia
kwenye gesti Bray iliyopoa maeneo Kimara , manispaa ya Kinondoni huku
chanzo cha kifo bado hakijawekwa wazi hadi uchunguzi utakapokamilika na
maiti huyo amehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala
News
Sunday, May 8, 2016
0 Response to " Mauaji Gesti ..Meya Ataka Gesti zifungwe Kamera za Siri..."
Post a Comment