Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Tawala
Bora, Angela Kairuki amewataka wahitimu wa Chuo cha Utumishi Umma
nchini (TPSC) kutojihusisha na masuala ya ufisadi, rushwa na matumizi
mabaya ya madaraka kazini badala yake wawe wachapakazi
watakapowatumikia Watanzania.
Kairuki alitoa kauli hiyo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa
wa Mbeya, Amos Makalla alipomwakilisha waziri huyo kwenye mahafali ya
24 ya chuo hicho yaliyofanyika tawi la Mbeya.
Alisema wakati Serikali ya awamu ya tano ikiendelea kupambana na
watumishi hewa, mafisadi na wazembe kazini, wahitimu katika chuo hicho
wahakikishe wanakwenda kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia kanuni,
sheria na taratibu za utumishi popote watakapoajiriwa.
“Huu ni wakati wenu kuonyesha utofauti kati ya aliyehitimu chuo na
kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, yule ambaye hajapitia chuo chochote,
lakini yupo ofisini utendaji kazi wake unadhihirisha kuwa hakustahili
kuwapo mahali hapo,” alisema
News
Sunday, May 8, 2016
0 Response to "Wahitimu Chuo cha Utumishi wa Umma Waonywa"
Post a Comment