Rais John Magufuli ametetea uamuzi wake wa kuwatimua baadhi ya watumishi
wa umma wanaokiuka maadili akisema anataka kuirejesha nchi kwenye
mstari.
Rais amesema hayo leo alipozungumza na waumini katika misa ya Jumapili
katika Kanisa Katoliki parokia ya Tokeo la Bwana Burka jijini Arusha.
Amesema watu katili ni wale ambao walikuwa wanawaibia Watanzania na kuwanyonya wanyonge.
Amesema analazimika kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi si kwamba ni
katili, bali lengo ni kuwatumikia Watanzania na kuirejesha nchi kwenye
mstari.
Rais huyo aliyejibatiza “mtumbua majipu”, amesema Tanzania ni taifa
tajiri, hakuna sababu ya wananchi kulalamika kila kona, kwani kuna ardhi
ya kutosha, madini ya kila aina, wanyama wa aina mbalimbali ambao
baadhi wameanza hadi kupelekwa nje.
"Ninapochukua hatua nataka kuweka Tanzania iliyonyooka, mimi tayari
nimesema nimejitoa sadaka kwa watanzania hasa wanyonge," alisema
News
Sunday, May 8, 2016
0 Response to " Rais Magufuli Atetea Uamuzi wake wa Kutimua Wafanyakazi"
Post a Comment