Baada ya wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kuufungia wimbo
wa Snura, Chura jana, muimbaji huyo anaonesha kutoshtushwa na hatua hiyo
hasa kutokana na support anaiyopata kutoka kwa mashabiki wake.
Kwa ufupi haoneshi stress, walau kwa kile alichokiandika kwenye
Instagram. “Ingekua ndio hela leo ningekua bilionea lo!!! Nawapenda sana
kwakweli na nawatakia usiku mwema,” aliandika Snura kwenye Instagram.
Aliongeza hashtag: #utaipenda2_ndimuimekolea_malimao_kama__210_habarizetuwanazo_ilazaohatuna.”
Pamoja na wimbo huo kufungiwa kuchezwa kwenye redio na TV, Snura aliagizwa kuhakikisha amefuta video zake zote mtandaoni
entertaiment
Wednesday, May 4, 2016
0 Response to "Majibu ya Snura baada ya Chura wake Kupigwa Nyundo na Serikali"
Post a Comment