Vyombo vya habari vya asilia hususani magazeti vinakufa. Hivi sasa
vvyombo hivyo vinajikongoja kutokana na mauzo hafifu na mdororo wa
mapato kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi.
Ila wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua,
wanaoperuzi mtandaoni humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando,
utafiti wa Pew Research Centre unaeleza.
Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 (“State of the
News Media 2015,”) imeonesha kwamba katika vyombo vya habari vya
karatasi (print media), Digitali na TV, imeonesha Dhahiri kwamba
magazeti yanaelekea kuzimu.
Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa
mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini,
ambapo gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa
nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa
mitandaoni
News
Wednesday, May 4, 2016
0 Response to "Mitandao yaharibu soko la magazeti, takwimu zaonyesha magazeti yanapitwa na wasomaji wa mitandao"
Post a Comment