MAYANJA: KIIZA, JUUKO, WAMESABABISHA SIMBA KUTUPWA NJE FA CUP

blogger templates
Safari ya Simba kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kupitia kombe la FA (Azam Sports Federation Cup) imehitimishwa na vibonde wa ligi ya kuu Coastal Union kwa kuchapwa bao 2-1 kwenye mchezo wa robo fainali uliochezwa Jumatatu April 11 kwenye uwanja wa taifa.
Kocha wa Simba Jackson Mayanja anasema wacheaji wake hawakucheza vizuri huku lawama nyingi akizielekeza kwa mshambulizi Hamisi Kiiza na mlinzi wa kati Juuko Murshid kwa kuchelewa kurudi kutoka Uganda walikoenda kuitumikia timu yao ya taifa.
“Wachezaji hawakucheza vizuri kama walivyotakiwa kucheza, wamepoteza nafasi nyingi za wazi tunatakiwa kujilaumu wenyewe na si vinginevyo”, Mayanja alisema baada ya kupoteza mchezo wake wa pili tangu alipojiunga na Simba”.



 http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2016/02/Mayanja-J-1.jpg


Mayanja pia amelalamikia suala la wachezaji wake wawili wa Uganga Hamisi Kiiza na Juuko Murshid kuchelewa kurudi kujiunga na timu baada ya kumaliza majukumu yao ya kuitumikia timu ya taifa kwenye mchezo wa kutafuta nafasi ya kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) 2017.
“Unajua kila siku nawaambia watu maandalizi ya timu yanatakiwa kuwa ni ya timu nzima, kama kunawachezaji wanatumikia timu zao za taifa wanapaswa kurudi mapema. Kama mwalimu siwezi kujenga timu kupitia mchezaji mmoja au wawili Juuko na Kiiza wamekuja siku chache kabla ya mechi kwahiyo walikuwa na siku chache za kufanya mazoezi na timu”, anasema Mayanja kocha wa zamani wa Coastal Union.
“Huwezi kuwaanzisha wacheaji kama hawa kwenye mechi, na mwalimu mwinge asingewaweka hata kwenye benchi lakini kwasababu kikosi chetu si kukubwa sana ndiyo maana nikawaweka kwenye benchi, lakini siyo sahihi wachezaji wakienda kwenye mechi za kimataifa wanakaa”, alisisitiza Mayanja ambaye baadaye alimwingiza Kiiza kuchukua nafasi ya Lyanga licha ya kumuanzishia benchi.
“Niliwaweka benchi kwasababu timu inawachezaji wachache kutokana na wengi kuwa majeruhi kwenye nafasi kadhaa. Lakini wakati mwingine ni matokeo ya mpira tunapaswa kukubali.”




0 Response to "MAYANJA: KIIZA, JUUKO, WAMESABABISHA SIMBA KUTUPWA NJE FA CUP"

Post a Comment