UONGOZI wa Azam FC umezuia safari ya kiungo wake Farid Mussa (pichani) kwenda Ubelgiji kwa majaribio ya kucheza soka ya kulipwa hadi amalize mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia Aprili 19.
Awali, makubaliano kati ya wakala wa Farid na Azam ilikuwa ni mchezaji huyo aondoke baada ya mchezo wa kwanza na Esperance uliofanyika Jumapili Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Farid alifunga bao moja na kuseti moja katika ushindi wa 2-1 na baada ya hapo, benchi la Ufundi chini ya kocha Muingereza, Stewart Hall limeona linamuhitaji kinda huyo kwa mchezo wa marudiano.
Mbali na Farid, kiungo Himid Mao pia anatarajiwa kwenda Denmark kwenda kujaribu bahati yake.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema kwamba wameiomba klabu inayomtaka Farid kwa majaribio imsubiri kwa wiki moja zaidi.
“Awali Farid Mussa alitakiwa kuondoka mara moja kwa ajili ya majaribio hayo, lakini tumewaomba wenzetu wanaomtaka wamuache hadi amalizie mechi yetu ya pili dhidi ya Esperance na wamekubali, hivyo Farid ataondoka baada ya mechi hiyo,” alisema.
0 Response to " HABARI MOTOMOTO HABARI ZA NYUMBANI AZAM YAMZUIA FARID KWENDA ULAYA HADI WAMALIZANE NA ESPERANCE AZAM YAMZUIA FARID KWENDA ULAYA HADI WAMALIZANE NA ESPERANCE"
Post a Comment