MFUNGAJI wa mabao yote ya Coastal Union ikiilza Simba SC 2-1 jana na kuitupa nje ya michuano ya michuano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup leo ameomba tena kusajiliwa Yanga.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 na klabu ya Cotton Sport ya Gorua, Youssouf Soba alikuwa Yanga mwishoni mwa mwaka jana kwa majaribio, lakini hakusajiliwa.
“Nilikwenda Yanga kuomba kusajiliwa mwaka jana, nikafanya majaribio, lakini kocha akasema mimi ni mchezaji mzuri ila nafasi za wachezaji wa kigeni zimeisha,”amesema Youssouf Soba akizungumza na,bin zubeir
Soba aliyasema hayo mara tu baada ya mechi hiyo ya Robo Fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na akasema hata kama Azam wanamtaka, yuko tayari kuzungumza nao.
Sabo alifunga bao la kwanza dakika ya 19 kwa shuti la mpira wa adhabu umbali wa mita zaidi ya 20 na kutinga nyavuni moja kwa moja likimpita kipa Muivory Coast, Vincent Angban, kabla ya Mganda Hamisi Kiiza kutokea benchi kipindi cha pili na kuisawazishia Simba dakika ya 47.
Hata hivyo, Sabo tena akaifungia Coastal bao la ushindi kwa penalti dakika ya 85, kufuatia beki Novaty Lufunga kumuangusha kwenye boksi mshambuliaji Ally Ahmed ‘Shiboli’.
0 Response to "HABARI ZA NYUMBANI ALIYEWAZURU SIMBA JANA AOMBA TENA KAZI YANGA ALIYEWAZURU SIMBA JANA AOMBA TENA KAZI YANG"
Post a Comment