Mzozo wa kidiplomasia unatokota baada ya Waziri mkuu wa Uingereza, David
Cameron, kunaswa kwenye Kamera akimwambia Malkia Elizabeth wa Pili kuwa
viongozi wa mataifa mawili yenye ufisadi mkubwa kote duniani Nigeria na
Afghanistan watakuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika kongamano la
kupambana dhidi ya zimwi la ufisadi litakalofunguliwa siku ya Alhamisi
mjini London.
Matamshi hayo ya Cameron yalitolewa katika kasri la Buckingham bw
Cameron alipokuwa amekwenda kumtembelea malkia Elizabeth katika sherehe
ya kuadhimisha miaka 90 ya kuzaliwa kwake.
Aidha Cameron alieelezea malkia Elizabeth jinsi mataifa hayo yalivyosakamwa na viongozi mafisadi.
Kiongozi wa kanisa la kianglikana Askofu mkuu wa Canterbury Justin Welby
aliyekuwa na viongozi hao wawili anasikika akimkumbusha Waziri mkuu bw
Cameron kuwa rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari si mfisadi.
Afghanistan iliorodheshwa katika nafasi ya 167, nafasi moja pekee mbele
ya Somalia na North Korea, katika orodha ya 2015 ya shirika la kupambana
na ufisadi duniani Transparency International .
Nigeria iliorodheshwa katika nafasi ya 136
News
Tuesday, May 10, 2016
0 Response to "Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron Anaswa Akisema Nigeria ni Vinara wa Rushwa Duniani"
Post a Comment