Ni hotuba ya Rais Magufuli akiwa Arusha kwenye kuweka baraka zake kwenye
majengo mapya ya PPF ambapo kwenye hotuba yake iliyochekesha watu wengi
aliongelea pia ishu ya madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania
pekee lakini nchi zinazotambulika kuyauza duniani ni India na Kenya.
President Magufuli alisema :
‘Siku nyingine hakuna ubaya hata NSSF mkawa ndio wawekezaji wakubwa wa
Tanzanite mkawa mnanunua Tanzanite kutoka kwa vijana hawa badala ya kuwa
inavushwa mpaka Kenya na kwenda Kenya, badala ya Tanzania kuwa ya
kwanza kuuza Tanzanite duniani inajitokeza India alafu inafata Kenya‘
‘Unajua saa nyingine watu wanatuona Watanzania sijui tukoje, huyu
shetani aliyetulaani sisi Watanzania kwanini asife? hata hatuhurumii
kidogo? basi kama ni kuswali na kusali tusali sana ili tubadilike,
tuthamini mali yetu kwa ajili ya vizazi vyetu‘
News
Tuesday, May 10, 2016
0 Response to " AUDIO: Rais Magufuli ‘Huyu Shetani Aliyetulaani Watanzania Kwanini Asife?’"
Post a Comment