Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Jakaya Kikwete amekuwa
miongoni mwa viongozi wa ngazi za juu katika ukanda wa Jumuia ya Afrika
Mashariki kuhudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa mama wa Taifa la
Kenya Bi Lucy Kibaki aliyefariki akiwa na miaka 82.
Marehemu Lucy Kibaki ametajwa na wanaomjua kama kiongozi aliyetetea
mazingira safi ya kifamilia na alikuwa tayari kufanya kila jambo
kuhifadhi utu na wema katika familia.
Kikwete ambaye aliwasilisha ujumbe wa Rais John Pombe Magufuli alisema
kifo cha mama Lucy kibaki kimetokea wakati mchango wake ukiwa bado
unahitajika katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto waliohudhuria
mazishi ya Bi Kibaki eneo la Bunge la Odhaya kaunti ya Njeri wamemtaja
marehemu kama kiongozi aliyekuwa tayari kuhudumia taifa la Kenya
News
Saturday, May 7, 2016
0 Response to " Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Ahudhuria Mazishi ya Lucy Kibaki nchini Kenya."
Post a Comment