Msanii Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake 'Achia
boy' amefunguka na kusema kuwa ameamua kumuweka wazi mpenzi wake ili
kupunguza usumbufu kutoka kwa watoto wa kike.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio, Ommy
Dimpoz alidai kuwa kufanya hivyo ni kupunguza kasi ya watoto wa kike
ambao wamekuwa wakimsumbua na kumtaka kimapenzi.
"Unajua saizi nimeamua kumuweka wazi mpenzi wangu ili wajue yupo na
kupunguza usumbufu kwa watoto wa kike ambao wanadhani labda niko single,
japo yupo mbali lakini kufanya hivyo inasaidia" alisema Ommy Dimpoz
Mbali na hilo Ommy Dimpoz alisema mpenzi wake huyo kwa sasa anasomea
udaktari nchini uingereza na kudai ni mtu wa Afrika Mashariki.
entertaiment
Wednesday, May 11, 2016
0 Response to "Nimemuweka Wazi Mpenzi Kupunguza Usumbufu - Ommy Dimpoz"
Post a Comment