Msanii Hawa ambaye aliimba na Diamond kwenye wimbo wa nitarejea, amesema
kwa sasa mume wake ndiye mtu muhimu zaidi maishani mwake kwani
amembadilisha maisha yake.
Hawa ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo
kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa wakati anakutana na
mume wake huyo ambaye anadaiwa kumbadilisha mpaka dini na kuwa mkristo,
alikuwa kwenye hali mbaya kwa ulevi.
“Mume wangu ndio kitu kikubwa sana kwa sababu kanibadilisha katika njia
nyingi sana, kipindi ambacho nalewa kwa sababu nilikuwa sikumbuki hata
kuoga watu wananisema kabisa huyu kawa teja, sikumbuki kufanya kitu
chochote mi nakumbuka kulewa tu lakini Lordvick alijitajahidi kwa ahali
yoyote kunifanya mimi nionekane katika hali ya usichana, na nilijisikia
vizuri nikahisi yeye ndo ananifaa”, alisema Hawa.
Hawa ambaye kwa sasa bado anaendelea na shughuli za muziki na hivi
karibuni alikiri kuhitaji uongozi wa kumsimamia kazi zake, amesema yupo
na mume wake huyo kwa ajili ya upendo aliounyesha na kumjali, lakini si
pesa.
News
Wednesday, May 11, 2016
0 Response to ""Nilikuwa Nalewa Mpaka Nasahau Kuoga"- Hawa wa Nitarejea Afunguka"
Post a Comment