Msanii wa filamu nchini Ray Kigosi amefunguka na kusema kuwa yeye furaha
yake ni kuona vijana wenzake wakifanikiwa na kupiga hatua kimaendeleo.
Ray Kigosi amewaasa vijana wenzake kuwa wasikae wakategemea kuwa
viongozi wa siasa wanaweza kuja kuwabadilishia maisha yao bali amewataka
kuwa na jitihada binafsi kwani huo ndiyo msingi mkubwa wa mustakabali
wa maisha yao.
“Furaha yangu ni kuona kijana mwenzangu ukifanikiwa na kupiga hatua
kimaendeleo, pambana achana na mambo yasiyo na msingi ukitaka kufanikiwa
katika ndoto zako fanya vitu vigumu kufanyika. Fanya kitu ambacho
mwingine hawezi kufanya, hakuna kiongozi yeyote wa nchi atakayekuja
kuyabadilisha maisha yako isipokuwa ni jitihada zako mwenyewe huo ndio
msingi mkubwa wa mustakabali wa maisha yako.
entertaiment
Saturday, May 7, 2016
0 Response to "Msanii Ray Kigosi Aibuka na Kutoa Soma Hili Kwa Vijana Kuhusu Viongozi wa Nchi na Siasa zao"
Post a Comment