Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umesema kutozingatia
sheria za barabara za mradi wa mabasi hayo, kwa vyombo vingine vya moto
vimesabisha ajali 14 wakati madereva wa mabasi hayo wakiendelea na
mazoezi kwa ajili ya kuelekea kipindi cha mpito cha mradi kinachotarajia
kuanza hivi karibuni.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Mhandisi Ronald Rwakatale amesema
kuwa ajali hizo zimejitokeza wakati madereva wa mabasi ya mradi
wakifanya mazoezi na kisha vyombo vingine vya moto viingilia barabara
zake na kusabisha ajiali hizo.
Amesema ajali hizi ni matokea ya vyombo vingine vya usafiri kama magari
madogo, daladala, bodaboda na waenda kwa miguu wamekuwa wakiingilia
barabara za mabasi hayo na kusabisha ajali kutokana na kwamba barabara
hizo haziruhusu mabasi hayo kupisha na vyombo vingine.
Mhandisi Rwakatale amesisitiza kuwa barabara za mabasi hayo ambazo ni za
zege zimejengwa mahususi kwa ajili ya mabasi hayo hivyo madereva wa
vyombo vingine wanahitajika kuheshimu sheria zinazoongoza mradi huo na
kupita katika barabara walizotengewa na watakaokiuka sheria itachukua
mkondo wake.
Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka unatarajiwa kuanza kipindi cha mpito
mwezi huu wa Mei kutoa huduma ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es
Salaam
News
Saturday, May 7, 2016
0 Response to " Idadi ya Ajali zilizojitokeza wakati wa Majaribio Mabasi yaendayo Haraka"
Post a Comment