Mrembo huyo aliyeuza nyago kwenye Video ya Wimbo wa Kwetu wa msanii wa Diamond, Irene’ Lynn’.
Mrembo ambaye wiki mbili zilizopita aligeuka gumzo baada ya kudaiwa
‘kuchepuka’ na staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Irene’
Lynn’ kisha kuleta mtikisiko kwa mpenzi wa msanii huyo, Zarinah Hassan
‘Zari The Boss Lady’ amefunguka kuhusu ishu hiyo.
Akizungumza wikiendi iliyopita baada ya kubanwa aseme ukweli kama
anatoka kimapenzi na Diamond, mrembo huyo aliyeuza nyago kwenye Video ya
Wimbo wa Kwetu wa msanii wa Diamond aitwaye Raymond alisema kuwa hata
yeye ishu hiyo inamshangaza.
Irene alisema siku zote watu hawajiamini wanapomuona msichana mzuri
akifanya kazi na mtu fulani na mara nyingine humwekea wivu na kuibua
mambo mengine. Irene aliweka wazi kuwa kilichompeleka Wasafi ni kufanya
kazi ya Wimbo wa Raymond na hakuna kingine kilichoendelea.
“Mkataba wangu na Diamond uliisha baada tu ya kufanya video ya msanii
wake,” alisema Irene. Mrembo huyo alitiririka kuwa ishu hiyo inamtesa na
kumsumbua kwa sababu watu wengi wanajua kuwa ni kweli ametembea na
Diamond, jambo ambalo si kweli.
Skendo ya Irene kutembea na Diamond ilileta mtafaruku mkubwa kwenye
familia ya mwanamuziki huyo kiasi cha dada wa mwanamuziki huyo, Esma
Platnumz, kuingia kwenye mgogoro mzito na Zari ikielezwa kuwa mrembo
huyo ni rafiki yake na alijua kilichokuwa kikiendelea.
News
Tuesday, May 10, 2016
0 Response to " Mrembo Anayedaiwa Kutoka Kimapenzi na Mwanamuziki Diamond Afunguka"
Post a Comment