Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) iliyokuwa ikipinga kuondolewa kwa shitaka
la 8 la utakatishaji fedha linalomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Harry Kitilya na wenzake wawili.
Uamuzi huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Jaji Mfawidhi wa
Mahakama hiyo, Mheshimiwa Moses Mzuna alipokuwa akitoa majibu ya rufaa
iliyokuwa imekatwa na DPP.
“Ninafahamu kila kesi inaamuliwa kutokana na mazingira yake lakini
nimefuta rufaa hii kwa kuwa hoja zilizotolewa hazina nguvu kisheria”
alisema Jaji Mzuna.
Aidha Jaji Mzuna amefafanua kuwa hata kama amefuta rufaa hiyo lakini
upande wa Jamuhuri bado una nafasi ya kubadilisha shitaka au hati nzima
ya mashtaka inayowakabili washtakiwa hao.
Kwa upande wake Wakili Mkuu wa Serikali Timony Vitalis amekubaliana na
uamuzi uliotolewa na Mahakama hiyo juu ya pingamizi lake ingawa bado
anasimamia watuhumiwa kutofutiwa shitaka la utakatishaji wa fedha.
Naye Wakili wa Utetezi Majula Magafu amesema kuwa wao wanasubiri maamuzi
yatakayotolewa na Wakili wa Serikali ili wajue namna ya kuikabili kesi
hiyo
News
Friday, May 6, 2016
0 Response to "Miss Tanzania na bosi wa zamani wa TRA wachekelea uamuzi wa Mahakama Kuu"
Post a Comment