Kocha mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameiambia timu ya Simba
kwamba inalaana ndiyo sababu ya kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano
ya ligi kuu Tanzania bara kwa muda mrefu.
Julio anadai laana hiyo inatokana na uongozi wa Simba kumfukuza yeye
pamoja na kocha mkongwe Abdallah Kibadeni ‘Kin Kibadeni Mputa’ bila
kuwalipa stahiki zao.
“Wakati mimi na King Kibaden tunafukuzwa Simba, niliwaambia kwamba
,mnatufukuza huku tunadai mishahara yetu na hiyo itakuwa laana kwasababu
sisi tunafamilia kubwa ambazo zinatutegemea lakini wao walitufukuza
hihuni”, anasema Julio ambaye ameshawahi kuitumikia Simba kama mchezaji
na baadaye kama kocha.
“Niliweka nadhili kwenye ligi hii baada ya kuipandisha Mwadui lazima
niifunge Simba, mechi ya kwanza tulitoka sare, walichomoa goli. Haji
Manara akasema kuna goli walitufunga likakataliwa, safari hii tumekuja
kwenye uwanja wao waliouzoea na tumewafunga.”
“Tukubali kwamba timu ya Simba mbovu na mimi nitoe wito kwa viongozi wa
Simba, kama wanataka timu ifanikiwe lazima wawe wanatoa nafasi kwa
waalimu wasajili wachezaji. Haya mambo ya mtu mwenye nguvu ya pesa ndiyo
asajili wachezaji ni makosa kwasababu kitaalamu hata Mungu kazi
nyingine hazitaki ndiyo maana kazi ya kuua kampa Israel.”
“Nimefurahi sana kuifunga Simba kwasababu wanapokuwa hawana kocha
wananiita, wakipata kocha mzungu wa kumlipa pesa nyingi wananitimua tena
kwa matusi.”
Maneno hayo ya Julio yamekuja mara baada ya Mwadui kuichapa Simba kwa
bao 1-0 kwenye mchezo wa VPL uliochezwa Jumapili kwenye uwanja wa taifa.
News
Monday, May 9, 2016
0 Response to "Kocha Julio Adai Timu ya Simba Ina Laana Kubwa Sana"
Post a Comment