Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema atahakikisha anashinda mchezo huo ili Yanga iwe bingwa.
Mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Mwadui FC ni kesho
Jumapili na inasubiriwa kwa hamu ile mbaya. Itapigwa kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 68 ikifuatiwa na Simba yenye pointi
58, wakati Azam ina pointi 57. Yanga na Azam zimebakiwa na michezo
mitatu, huku Simba wakiwa nayo minne.
Simba ikishinda mechi zake zote ikiwemo hii na Mwadui, itafikisha pointi
70, hivyo Yanga na Azam zikipoteza mechi zake zilizobaki, Wekundu wa
Msimbazi wanaweza kuwa mabingwa.
Julio ambaye amewahi kucheza na kufundisha Simba, alisema hataleta
urafiki kwenye mchezo huo na amepanga kushinda ili Yanga ipate ubingwa
rasmi.
sports
Saturday, May 7, 2016
0 Response to "KOCHA Jamhuri Kihwelo 'Julio' Ajigamba..Lazima Tuifunge Simba"
Post a Comment