WCB imemzawadia gari jipya msanii wake, Harmonize.
Bosi wake, Diamond, ameandika kwenye Instagram: Kama nikusiivyo siku
zote ni juhudi na nidhamu yako ndio itayokufanya upate matunda ya kazi
yako….. Usiache unyenyekevu, kuheshimu mkubwa na mdogo, kumuomba na
kumshukuru Mwenyez Mungu kwa kila hatua ndogo Uipigayo…. Congrats kwa
your New Ride.”
Naye Harmonize hakuacha kuonesha furaha yake.
“Nichukue fursa fupi kuushukuru uongozi wangu mzima wa @wcb_wasafi
@mkubwafella @babutale @sallam_sk @ricardomomo @diamondplatnumz kwa
kunijali na kunithamini kijana wao wakanizawadia gari daaaaah furaha
niliyo nayo haielezeki,” ameandika msanii huyo.
“Kwakweli nina furaha na ninashukuru sanaa nina mengi ya kuongea lakini
sizani kama nikianza kuandika nitamaliza kubwa ni kwamba namshukuru
m/mungu nashukuru kwa kurudia tena uongozi wangu @wcb_wasafi kwa zawadi
lakini nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipo washukuru wazazi wangu walio
nizaa na kunilea hadi nikafikia hapa na shukrani za dhati ziwafikie
mashabiki zangu ambao wapo bega kwa bega kunisupport katika kazi zangu
pia mama naseeb umekuwa ukinisistiza na kunisihi jinsi ya kuishi na watu
@kendrah_michael.”
“Nimalize kwakusema ninashukuru sanaa na nina amini kuna mengi mazuri
zaidi yapo mbele ila asieshukuru na kidogo kamwe hatoshukuru na kikubwa
thanks #allah thanks #wcb #thanks #mashabiki.”
entertaiment
Saturday, May 7, 2016
0 Response to "Diamond na Kampuni yake ya Music WCB Yamzawadia Gari Jipya Harmonize"
Post a Comment