Klabu ya Coasta Union ya jijini Tanga itahitaji miujiza pekee ili iweze
kubaki katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao kutokana na hesabu
kuonesha kuwa tayari timu hiyo imeshuka daraja.
Miujiza hiyo inatokana matokeo iliyopata leo katika dimba la CCM
Kambarage mjini Shinyanga kwa kuchapwa mabao 2-1 na wenyeji Stand
United.
Mabao yote mawili ya Stand United katika mchezo wa leo yameupiwa wavuni
na Elias Maguli katika dakika ya 29 kwa njia ya penati baada ya mchezaji
wa Stand kuchezewa madhambi katika eneo la hatari, huku bao la pili
akilipachika katika dakika ya 46, muda mfupi baada ya kipindi cha pili
kuanza, kabla ya Coastal kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa said.
Kwa mabao hayo sasa mshambuliaji Elias Maguli amefikisha magoli 14 na
anakamata nafasi ya 4 katika orodha ya wafungaji wanaoongoza kwa mabao
mengi zaidi akitanguliwa na Amis Tambwe (20), Hamis Kiiza (19), Donald
Ngoma (16) huku akimuacha Kipre Tcheche na John Bocco wenye mabao 10
kila mmoja.
Matokeo haya yanaifanya Coastal kutangulia ligi daraja la kwanza huku
ikiwasubiri wenzake wawili kutokana na kuwa na point ambazo haziwezi
kuinasua kutoka katika nafasi tatu za chini hata kama itashinda mchezo
wake wa mwisho uliobaki.
Kwa upande wa mechi nyingine zilizopigwa leo, JKT Ruvu imeibwaga Ndanda FC kwa mabao 2-0, huku
Mgambo JKT ikiilazimisha sare ya bao 1-1 Mtibwa Sugar
Hesabu zinaonesha kuwa baada ya michezo ya leo Jumamosi, Coastal Union
imeendelea kubaki mkiani na point zake 22, ikiwa nyuma ya Mgambo JKT
iliyofikisha pointi 24 ikiwa na mechi 2 mkononi, Kagera Suga yenye point
25 na mechi 3 mkononi, na African Sports ikiwa na point 26 na mechi 2
mkononi.
Kwa upande wake JKT Ruvu kwa kiasi kikubwa imejinasua kutoka katika
dimbwi hilo la kushuka daraja baada ya ushindi wake wa leo ulioifanya
ifikishe pointi 29
sports
Saturday, May 7, 2016
0 Response to " Coastal Union Chali Yafungashiwa Virago Vyake na Kushuka Ligi Daraja la Kwanza"
Post a Comment