Watu watatu akiwemo raia wa Kenya wanashikiliwa na jeshi la polisi
mkoani Kilimanjaro baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya
Mirungi na Bangi kilo 54 na misokoto ya Bangi 4,500 ikisafirishwa kutoka
nchini Kenya kwenda mkoani Arusha.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Bw.Wilbrod Mutafungwa amesema
watuhumiwa hao wamekamatwa katika maeneo ya njia panda Himo wilaya ya
Moshi na Sanya juu wilaya ya Siha wakiwa wameficha madawa hayo ya
kulevya kwenye miili yao kuanzia maeneo ya tumboni hadi miguuni.
Amewataja waliokamatwa ni Vitalis Victor mfanyabiashara mkoani Arusha,
Naftal Mvoyi mkazi wa Voi nchini Kenya, Maulid Maulis mkazi wa Arusha
ambao walikuwa wakisafirisha Mirungi kilo 44 kwa kutumia magazeti na
gundi ya karatasi na kisha kuifunika kwenye nguo walizokuwa wamevaa
wakitokea nchini Kenya kuelekea jiji la Arusha.
Ripota wetu amefanikiwa kuzungumza na baadhi ya vijana wanaojihusisha na
matumizi ya madawa ya kulevya katika manispaa ya Moshi na kueleza
kwamba changamoto kubwa inayowabaili ni ukosefu wa ajira hali
inayowasababisha baadhi yao kujihusisha na matukio ya uhalifu.
Matumizi ya madawa ya kulevya yameathiri vijana wengi kiafya kutokana na
baadhi yao kushindwa kufanya shughuli za maendeleo na hivyo kulazimika
kujihusisha na matukio ya wizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
News
Monday, April 25, 2016
0 Response to " Watu Watatu Wakamatwa na Madawa ya Kulevya Aina ya Mirungi Mkoani Kilimanjaro"
Post a Comment