Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Aprili 27, 2016) jijini Dar es
Salaam kwa kuzingatia Kanuni ya 28(2) ya Kombe la Shirikisho. Wakati
mechi hiyo inavunjwa, Yanga ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1.
Pia Coastal Union imepigwa faini ya sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa
kuzingatia Kanuni ya 42(26) ya Ligi Kuu kutokana na vitendo vya vurugu
za washabiki wake wakati wa mechi hiyo. Pia TFF haitasita kufungiwa
uwanja huo iwapo vitendo hivyo vya vurugu za washabiki havitakoma.
Mwamuzi wa mchezo huo Abdallah Kambuzi amefungiwa mwaka mmoja wakati
Mwamuzi Msaidizi namba mbili Charles Simon ameondolewa kwenye ratiba ya
waamuzi. Adhabu hizo zimetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(1) ya Ligi
Kuu.
Mchezaji Adeyum Ahmed wa Coastal Union anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya
TFF kwa ajili ya hatua zaidi kutokana na kitendo chake cha kumpiga
kichwa Mwamuzi wa Akiba baada ya kutolewa nje. Hata hivyo, Ahmed
hakufanikiwa kutimiza azma hiyo baada ya Mwamuzi huyo kumkwepa.
Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya
14(13) ya Ligi Kuu kutokana na kutoingia vyumbani kwenye mechi hiyo ya
Kombe la Shirikisho.
Vilevile malalamiko ya Coastal Union kutaka mechi hiyo irudiwe yametupwa
baada ya Kamati ya Mashindano kubaini kuwa hayana msingi wowote
sports
Thursday, April 28, 2016
0 Response to "Timu ya Yanga yatinga Rasmi Fainali Kombe la Shirikisho...Coastal Union Imepigwa Faini"
Post a Comment