Mtoto mwenye umri wa miaka miwili amemuua mama yake mzazi kwa bahati
mbaya katika jiji la Milwaukee nchini Marekani, baada ya kuikuta bastola
nyuma ya gari walilokuwamo.
Mwanamke huyo kwa jina la Patrice Price alikuwa akiendesha gari la mpenzi wake ambaye anafanya kazi za kiusalama nchini humo.
Polisi wa Milwaukee wamesema kuwa mwanamke huyo alipigwa risasi moja
mgongoni ndani ya gari hilo ambalo pia kulikuwa na mama wa Prince ambaye
ni bibi wa mtoto huyo pamoja na mtoto mwingine wa mama mwenye umri wa
mwaka mmoja.
Mwezi mmoja uliopita mtoto mwenye umri wa miaka minne huko Florida
alimpiga risasi mama yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Jamie Gilt
katika tukio linalofanana na hilo japo mama huyo hakupoteza maisha.
Pichani ni marehemu Patrice Price
News
Thursday, April 28, 2016
0 Response to "Mtoto wa Miaka Miwili Amuua Mama yake Kwa Risasi"
Post a Comment