Marekani yazidi kushambulia Al Shabaab

blogger templates










 Jeshi la Marekani limesema kwamba lilitekeleza mashambulio ya anga nchini Somalia na kuwaua wapiganaji 12 wa kundi la Al Shabaab. Idara ya ulinzi imesema wapiganaji hao walitishia usalama wa maafisa wa Marekani ambao wanasaidia wanajeshi wa serikali ya Somalia.
Mashambulizi hayo yalitekelezwa Jumatatu na Jumanne ya wiki hii viungani mwa mji wa Kismayo kusini mwa Somalia. Jeshi la Marekani halijaelezea kwa kina tishio la Al Shabaab kwa maafisa wake



 


Wakaazi wa maeneo kulikofanyika mashambulio hayo wameambia BBC baadhi ya waliouawa walikua ni raia. Haya ndiyo mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani nchini Somalia dhidi ya kundi la Al Shabaab ambalo linashirikiana na mtandao wa Al Qaeda.
Wiki jana idara ya ulinzi ya Marekani ilisema kiongozi mmoja wa Al Shabaab Hassan Ai Dhoore alikua ameuawa kwenye shambulio la ndege isiyo na rubani. Wapiganaji hao wamekua wakitekeleza mashambulizi makali dhidi ya maafisa wa serikali ya Somalia, wanajeshi wa kigeni sawa na kulenga hoteli na migahawa katika mji mkuu Mogadishu.

0 Response to "Marekani yazidi kushambulia Al Shabaab"

Post a Comment