Baada ya ukimya wa muda mrefu sana wa wakongwe wa muziki wa Bongo Flava
story zilizopo mtaani ni kuwa Ferooz ni miongoni mwa wasanii wanaotumia
madawa ya kulevya na ndiyo sababu iliyompoteza kwenye reli ya muziki.
Kupitia Enewz Ferooz alikanusha tuhuma hizo na kudai kuwa misongo ya
mawazo ndo huwa inawapelekea wasanii kuingia katika matumizi hayo ya
madawa ya kulevya na kuwataka wengine wasifanye hivyo.
Ferooz amesema kuwa “Ni mara kumi upate UKIMWI kuliko uwe unatumia
madawa ya kulevya” lakini pia akaongezea kwakusema “Nawashauri watu
wengine pamoja na wasanii wenzangu wasije wakajaribu kufanya hivyo”.
News
Saturday, April 30, 2016
0 Response to "Madawa ya Kulevya yamponza Mwanamuziki Ferooz...Mwenyewe Asema Haya"
Post a Comment