Morogoro. Mwanafunzi wa chekechea wa Shule ya Msingi ya Dala iliyoko
Kata ya Mvuha, Erick Makale (6) amefariki dunia baada ya kusombwa na
mafuriko wakati akiogelea na wenzake kwenye Mto Mvuha mkoani hapa.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu, mwenyekiti wa kijiji hicho, Boi Lubegete alisema kuwa mwili wa Erick bado haujaonekana.
Lubegete alisema kuwa Erick alikuwa na wenzake watatu na waliingia
kuogelea mtoni baada ya kumaliza kazi ya kufua, lakini yeye aliingia
kwenye kina kirefu na ndipo aliposombwa na maji.
“Watoto wenzake walieleza kuwa baada ya Erick alijaribu kujiokoa kwa
kushika mti kando ya mto huo, lakini baadaye aliuachia na kuzama. Mpaka
leo bado mwili wake haujapatikana,” alisema Lubegete.
Wakati huo huo Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini imetoa msaada
wa vyakula vyenye thamani ya Sh3.5 milioni kwa kaya 86 zilizoathiriwa na
mafuriko.
News
Wednesday, April 27, 2016
0 Response to "Maafa ya Mafuriko..Mwanafunzi Asombwa na Maji Akiogelea Morogoro"
Post a Comment