THE INDUSTRY MUSIC LABEL
TAARIFA KWA UMMA
THE INDUSTRY YATAMBULISHA RASMI WASANII WAKE MBELE YA WAANDISHI WA HABARI
Kampuni ya Muziki ya The Industry iliyoko chini ya Producer wa Music
Nahreel siku ya leo tarehe 6 mwezi wa Tano 2016 imewatambulisha
wanamuziki wake watatu wapya ambao watakuwa chini ya usimamizi wa label
hiyo.
Kati ya wasanii hao watatu wawili ni wake kike ambao ni Rosa Ree na Seline na Wakiume mmoja ajulikanae kwa jina la Wildad
The Industry wamesema kazi zao zitaanza kuchezwa redioni na kwenye TV
siku si nyingi ambapo jumatatu ijayo wataachia wimbo wa Seline pamoja
na Video yake
The Industry ni studio na kampuni ya muziki ambayo ipo chini ya kundi la
music lenye Mafanikio makubwa la Navy Kenzo ikisimamiwa na Producer
Nahreel na msaidizi wake Aika Marealle
Wasanii Baadhi Waliokwisha fanya kazi na Studio ya The Industry mpaka
sasa toka kuanzishwa kwake hivi karibuni ni Diamond Platnumz na wimbo
wake wa Nana, Nikki wa Pili na wimbo wa Baba Swalehe, Joh Makini na
nyimbo zake kama Don’t Bother na nusu nusu.
Imetolewa na,
The Industry PR
Nahreel Akiongea na Waandishi wa Habari , Kulia kwake ni Seline , Kushoto ni Rose Ree na Aika
0 Response to "The Industry Yatambulisha Rasmi Wasanii Wake Mbele ya Waandishi wa Habari leo"
Post a Comment