Kiukweli huyu katibu mkuu hajui hata pa kuanzia Chama kinaonesha dalili za kuifuata TLP na UDP sioni harakati zake ki ukweli CHADEMA ilikosea sana Dr. Mashinji ni unpopular figure hata akitembea kwa miguu Karikoo hakuna wa kumshitukia kuwa ni kiongozi.
Ukimya wake ni hatari kwa mustakabari wa chama kwani watu wasiokuwa na vyeo kama akina Lowassa ndo wamekuwa msaada mkubwa kukisemea chama kwa sasa. Anaonekana kabisa ni uteuzi ambao ulikosewa na ni mtu asiyekua na ushawishi ndani ya chama.
Kutoka kwenye nchi ya viwanda mpaka nchi ya majipu alikuwa ana mengi ya kuongea lakini yupo kimyaa wakisubiri kuzungusha mikono mwaka 2020.
Huku serikali ya Magufuli ikijisafishia njia inaonekana haitapata upinzani mwaka 2020 kutokana na uchakavu wa CHADEMA.
By Allen Snr
0 Response to "CHADEMA na Katibu Mkuu mfu..Ukimya Wake ni Hatari kwa Mustakabari wa Chama"
Post a Comment