Klabu ya Yanga ya Tanzania
imepangwa kukutana na klabu ya Sagrada Esperanca Angola katika hatua ya
mtoano (16 bora) ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Yanga itaanzia nyumbani kati ya tarehe 6
hadi 8 mwezi Mei, na marudiano itakuwa nchini Angola kati ya tarehe 17
na 18 mwezi huohuo.
Yanga imefikia hatua hiyo baada ya
kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Mabingwa Barani Afrika na Al Ahly
baada ya kufungwa 2-1 katika mchezo wa marudiano uliopigwa jana nchini
Misri.Jumla
ya timu 8 zilizotolewa katika michuano hiyo pamoja na Yanga zimeshushwa
katika michuano ya Kombe la Shirikisho na kukutana na timu nyingine 8
zilizofuzu kutoka raundi ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho.
Shirikisho la Soka Barani Afrika limeendesha droo muda mfupi uliopita na matokeo ya droo hiyo ni kama ifuatavyo.
Michezo yote ya kwanza itachezwa kati ya tarehe 6 na 8 mwezi Mei na marudiano ni kati ya tarehe 17 na 18 mwezi Mei.
Kati ya timu hizo 16, timu nane
zilizofuzu 8 bora kupitia michuano hiyo ni Esperance (Tunisia), Stade
Gabesien (Tunisia), FUS Rabat (Morocco), Misr Makkassa (Egypt),
Esperanca (Angola), CF Mounana (Gabon), Kawkab (Morocco) wakati Medeama
(Ghana).
Timu zilizofikia hatua hiyo kutokana na
kutolewa katika michuano ya Mabingwa Afrika ni TP Mazembe (DR Congo),
Etoile du Sahel (Tunisia), El Merreikh (Sudan), Stade Malien (Mali), MO
Bejaia (Algeria), Ahli Tripoli (Libya), Mamelodi Sundowns (South Africa)
na Young Africans (Tanzania)
0 Response to "YANGA YAPANGIWA WAANGOLA KOMBE LA SHIRIKISHO"
0 Response to "YANGA YAPANGIWA WAANGOLA KOMBE LA SHIRIKISHO"
Post a Comment