Kwa mujibu wa historia, Zaidi ya miaka
1937 imepita kutoka kuzaliwa mmoja wa Wanafunzi wa Kiongozi wa Umma wa
Kiislamu Mtume Muhamad (S.A), Imamu Ally ambaye katika kipindi cha
uongozi wake alisifika zaidi kwa mambo makuu manne.
Moja ya jambo kubwa alilosifiwa katika
utawala wake ilikuwa ni utawala uliojaa na imani ya kumuamini Mungu na
kumtegemea kwa kila kitu, kwa mujibu wa mapokeo ya Dini ya Kiislamu
imeandikwa kuwa mtu mwenye hofu ya Mungu huwa makini sana na jambo lake;
kuhusu jambo la Ufisadi Mwanafunzi huyo wa Mtume alilipiga vita wakati
wa utawala wake.
Mambo hayo mawili yanamfanya Kiongozi
Mkuu wa Waislamu wa Dhehebu la Shia la Ithnasheri ya Tanzania Sheikh
Hemed Jalala kumfananisha kwa kiasi kikubwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika kila jambo kwenye utawala
wake
0 Response to "RAIS MAGUFULI AFANANISHWA NA MWANAFUNZI WA MTUME MUHAMAD (S.A"
Post a Comment