Akiongea kwenye kipindi cha Nirvana, kinachoruka kupitia EATV, Wolper
alisema ‘nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule, sasa hivi
nimeshakuwa na mchumba’.
“Nilikuwa navaa vile kutokana na wakati ule ulivyokuwa. Kuna watu walikuwa wanapenda, lakini sasa hivi nimeshakuwa mchumba wa mtu. Ni kweli lazima nivae gauni, kwahiyo mtu unatakiwa ujibadilishe wewe mwenyewe usisubiri kubadilishwa,” aliongezea.
Wolper aliendelea kusema, “hata hivyo bado sijaacha kabisa, kidogo unakuwa unagusia mashabiki zako wanakuwa wanakupenda.”
Hata hivyo Wolper japo amekiri kuwa na mchumba mpya kwa sasa lakini
hayupo tayari kuweka mahusiano yake hadharani kama mwanzo alivyokuwa
anafanya.....
0 Response to "Mrembo Jack Wolper Afunguka Sababu za Kuacha Kuvaa Nguo za Kiume"
Post a Comment