MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki ametaka
kufanyika uchunguzi wa kuwabaini na kuwakamata kisha kuchukulia hatua kali za
kisheria watu wanaokatisha wanafunzi masomo yao kwa kuwapa mimba.
Sadiki aliongeza kwa kusema kuwa serikali haitasita kuwachukulia
hatua za kinidhamu walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari, ambao ni
hodari kutaja wanafunzi wenye ujauzito bila kuwataja wahusika au hatua
zinazochukuliwa kukomesha vitendo hivyo.
Akizungumza na walimu wa shule za msingi, sekondari,
watendaji wa ngazi zote za Halmashauri ya Wilaya ya Same, mkuu wa mkoa alitaka
wasichana walindwe ili kutimiza ndoto zao.
“Mkuu wa wilaya hakikisha wanaume hao wanakamatwa na
kufikishwa katika vyombo vya dola, ni aibu nasikia wengine ni viongozi, walimu…
mnaharibu maisha ya watoto wetu bure, mkubali msikubali watoto wa kike ndiyo
wanaongoza kufanya vizuri katika mitihani, angalia kidato cha nne na sita,”
alisema Sadiki.
Alisema ni jambo la ajabu kwa walimu kwa kushirikiana na
waratibu elimu kata kutofuatilia mienendo ya wanafunzi wanaporejea nyumbani, na
kutaka taarifa iandaliwe kwa ajili ya hatua zaidi.
0 Response to "Mafataki kukiona cha moto Kilimanjaro"
Post a Comment