ABIRIA wenye mizigo mikubwa na samaki wasiohifadhiwa vizuri, hawataruhusiwa kupanda mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo imelenga kuwapunguzia bugudha na shombo watumiaji wengine wa vyombo hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayoendesha mabasi hayo UDA-RT, David
Mgwasa, aliyasema hayo alipozungumza na gazeti hili jana, alipoulizwa
kuhusu abiria wanaosafiri na samaki kutoka Kituo cha Kivukoni kwenye
Soko la Kimataifa la Samaki na kwingineko.
Alisema ili kuepuka abiria wengine kubugudhiwa na kupata shombo ya
samaki, abiria wenye mizigo mikubwa hawataruhusiwa na wenye samaki
lakini watakaohifadhi samaki vizuri kwenye ndoo safi, watatumia huduma
hiyo.
UDA-RT ilianza kutoa huduma ya usafiri kwa mabasi hayo kuanzia Jumanne
wiki hii na inaendelea kusafirisha abiria bure hadi Jumapili, lengo
likiwa ni kutoa muda wa elimu ya namna ya kutumia mabasi hayo.
Aidha, Mgwasa alisema leo mabasi hayo yataanza saa 12 asubuhi mpaka saa tano usiku.
Alisema kuwa wamekuwa wakiongeza muda zaidi nyakati za usiku, kutokana
na changamoto za nyakati hizo, kabla ya kuanza rasmi huduma hiyo
Jumatatu.
Kwa mujibu wa Mgwasa, kwa sasa kuna mabasi 80 barabarani katika njia
zote. Kesho kutwa, Jumapili, UDA-RT itahakikisha mabasi yote 140
yanakuwa barabarani, kufanya majaribio ya kubadilisha abiria.
“Tunazidi kuongeza muda wa kulaza mabasi, na pia Jumapili tutatoa mabasi
yote, kwani mbali na kuangalia suala zima la abiria na uendeshaji pia
tunaangalia namna nzuri ya madereva kubadilishana, maana haiwezekani
dereva akaamka saa 10 aendeshe hadi usiku,” alisema.
Uwezo wa magari Mgwasa alisema mabasi makubwa yana uwezo wa kubeba abiria 150 kwa safari moja na madogo yanabeba abiria 90.
Wingi wa watu unaoonekana kwenye mabasi hayo kwa sasa, unatokana na
kuruhusu mabasi machahe kuwa barabarani. Kadi (tiketi) Mgwasa alisema
kadi maalumu ambazo zitauzwa kwa Sh 5,00 kwa bei ya promosheni, itakuwa
ikitumika kwa mtu mmoja wakati wa safari.
“ Mtu kama ana kadi moja na anasafiri na familia yake, kadi hiyo
itatumika kwa mtu mmoja na wengine watalazimika kukata tiketi, kwani
kadi itamruhusu mtu mmoja wakati wa kuingia na kutoka,” alisema
News
Friday, May 13, 2016
0 Response to "ZINGATIA Shombo ya Samaki Marufuku Mabasi ya Kasi Dar es Salaam"
Post a Comment