MTANGAZAJI wa Kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa kupitia EATV,
Joyce Kiria ameweka wazi kuwa hivi sasa yuko kwenye mikakati ya
kupunguza mwili wake ili asije kupoteza ndoa.
Akizungumza na Amani Joyce alisema, amekuwa akiuweka mwili wake sawa
ili usinenepe sana kwa kuwa hataki tena kuonekana mzee akawapa nafasi
wasichana ‘potabo’ wakaingilia ndoa yake na kuipoteza.
“Akuu!! Kisa cha kujizeesha na mwili hata ukitembea na mumeo uonekane
kama shangazi yake mimi sitaki kabisa, sasa hivi ni diet kwa kwenda
mbele kila kukicha nisije kuwapa madungaembe nafasi ya kuingilia ndoa
yangu,” alisema Joyce.
News
Thursday, May 12, 2016
0 Response to "Ubonge wa Mwili Wamtesa Joyce Kiria, Ahofia Kuipoteza Ndoa yake..."
Post a Comment