Jay Z analikamua limao lake mwenyewe pia.
Mtu wa karibu na familia hiyo, ameliambia jarida la US Weekly kuwa
rapper huyo, 46, anarekodi nyimbo zitakazoeleza upande wake wa
kilichotokea kwenye ndoa yake na Beyonce.
April 23, Queen Bey, 34, aliwashangaza mashabiki kwa video maalum
iliyorushwa na HBO pamoja na album ya Lemonade, inayoelezea tetesi za
muda mrefu za kusalitiwa na mume wake kwa mashairi kama: This is your
final warning / You know I give you life / If you try this s‑‑t again /
You gon’ lose your wife.”
Watu wanadai kuwa wawili hao walikuwa mbioni kuachana kabisa mwaka 2014
baada ya tukio maarufu kwenye lifti. May 2014, TMZ walivujisha video
inayomuonesha mdogo wake Beyoncé, Solange Knowles, akimshambulia Jay Z
wakiwa kwenye lifti baada ya kuhudhuria hafla ya Met Gala.
Vyanzo vinadai kuwa wanandoa hao waliweza kumaliza tofauti zao na sasa wako imara tena.
entertaiment
Wednesday, May 4, 2016
0 Response to "Ripoti: Jay Z Kuja na Album yake Atakayousema Ukweli Wake Kama Alivyofanya Beyonce Kwenye Lemonade"
Post a Comment