Rais John Magufuli amewataka Watanzania wasimuone katili kwa kuwafukuza
kazi baadhi ya watendaji wa Serikali, kwakuwa anataka kuirejesha nchi
kwenye mstari.
Akizungumza katika misa ya Jumapili kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya
Tokeo la Bwana Burka jijini Arusha, Rais Magufuli alisema watu katili ni
wale ambao walikuwa wanawaibia Watanzania na kuwanyonya wanyonge.
Dk Magufuli alisema analazimika kuchukua hatua ya kuwafukuza kazi si
kwamba ni katili, bali lengo ni kuwatumikia Watanzania na kuirejesha
nchi kwenye mstari.
Alisema Tanzania ni taifa tajiri, hakuna sababu ya wananchi kulalamika
kila kona, kwani kuna ardhi ya kutosha, madini ya kila aina, wanyama wa
aina mbalimbali ambao baadhi wameanza hadi kupelekwa nje.
“Ninapochukua hatua nataka kuweka Tanzania iliyonyooka, mimi tayari
nimesema nimejitoa sadaka kwa Watanzania hasa wanyonge,” alisema.
Aliongeza kuwa hatawaangusha Watanzania na hatabadilika, ataendelea
kusimama na kutetea haki za Watanzania maskini na siku zote atatembea na
maskini.
News
Monday, May 9, 2016
0 Response to " Rais Magufuli Asema yeye Siyo Katili, Anawatumikia Watanzania ili Kurejesha nchi Kwenye Mstari"
Post a Comment