Msanii Nuh Mziwanda ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake mpya
ambao amemshirikisha Alikiba amefunguka na kusema kuwa hata kama
ikitokea mpenzi wake huyo wa zamani akitaka kurudiana na yeye ni kitu
kisichowezekana kwa sasa.
Akizungumza kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na ting’a namba
moja kwa vijana Nuh Mziwanda amesema kuwa kwa sasa yeye amefunga ukurasa
wa mapenzi na Shilole hivyo hata ikitokea akataka kurudiana na yeye
hawezi kufanya hivyo kwani ameshaanza maisha mapya ambayo anaona ni ya
furaha zaidi.
Mbali na hilo Nuh Mziwanda ameeleza kuwa kwa sasa hataki tena maisha ya
kiki na skendo alizoita kuwa ni za ajabu ajabu bali anataka kujenga jina
lake kutokana na kazi zake kwenye muziki pamoja na kutengeneza muziki
kama ‘Producer’
entertaiment
Friday, May 6, 2016
0 Response to "Nuh Mziwanda Afunguka Kuhusu Kurudiana na Shilole"
Post a Comment