Samahani kwa Kuficha Picha , Sio Nzuri |
Habari kutoka Kaole; Majira ya saa 12 jioni jana, ilipita pikipiki eneo hilo ikiwa imepakiza watu watatu, dereva wa nne! Wanaume wawili, mwanamke na mtoto.
Walipofika eneo la darajani, porini kidogo, pikipiki ilipaki, watu wote wakashuka ndipo hatua za utekelezaji mauaji hayo zilianza.
Inadaiwa kwamba, Mama na mtoto wake walinyongwa Kwanza kabla ya kuchinjwa shingoni mithili ya kuku!
Lakini wakati mauaji hayo yakitekelezwa kulisikika makelele porini ambapo baadhi ya wananchi waliyoyasikia walielekea huko ndipo walipokutana na wauaji hao wakiwa na majambia yaliyoloa damu wakitokea porini.
Walipowaona watu hao walikimbia na kuacha pikipiki yao ambayo inashikiliwa Polisi. Katika eneo la tukio, mbali na pikipiki pia kulikutwa simu tatu za mkononi na mkoba wa mwanamke aliyeuawa.
Kwa mujibu wa taarifa, watu hao ni wageni Kaole na mpaka sasa bado miili yao haijatambuliwa!
Picha zinatish mno ndo maana hazijatumwa humu kama una ndugu yako mwenye mtoto wa kiume umri miaka 3-5 halafu kapotea mazingira ya kutatanisha jitahidi kufwatilia
0 Response to "Mauaji ya Kutisha Kaole Bagamoyo Jana Jioni..Mama na Mtoto Wachinjwa Kama Kuku"
Post a Comment