SIKU moja baada ya Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani bungeni, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), kudai
kuna uvunjifu wa sheria katika uhamishaji wa fedha zilizoidhinishwa na
Bunge, Tume ya Mipango imetoa ufafanuzi na kusema hakuna sheria
iliyovunjwa

Akizungumza mara baada ya kuzinduliwa
kwa Kitabu cha Muongozo kuhusu wa Usimamizi Rasilimali za Umma, Kaimu
Katibu Mkuu wa Tume ya Mipango, Florence Mwanry alisema madai
yaliyotolewa juzi na Mbowe bungeni si ya kweli.
“Wabunge ndio walipitisha wenyewe
Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015, ambayo inafafanua kuhusu uhamishaji wa
fedha kutoka kifungu kimoja kwenda kingine, hivyo uhamisho wa fedha
uliofanywa uko sahihi na hakuna sheria iliyovunja, wakaisome vizuri,”
alisema Mwanry.
Mbowe akizungumza na waandishi wa
habari juzi baada ya kususa Bunge, alitoa mfano wa bajeti ya maendeleo
iliyoidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
kwa mwaka wa fedha 2015/16, iliyokuwa ya Sh bilioni 883.8, ambapo kati
ya fedha hizo, fedha za ndani zilikuwa ni Sh bilioni 191.6.
Alisema inashangaza kuwa hadi kufikia
Machi 2016, Wizara ilikuwa imeshapokea kutoka Hazina Sh bilioni 607.4,
ambazo ni fedha za ndani, tofauti na ilivyopangwa kuwa fedha za ndani ni
Sh bilioni 191.6. Mbowe alidai kuwa hiyo inaonesha kuwa kuna ongezeko
la fedha zilizotolewa na Hazina hadi kufikia Machi 2016, ikilinganishwa
na fedha zilizoidhinishwa na Bunge.
Akitoa ufafanuzi, Mwanry ambaye ni
Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Mipango, alisema Sheria ya Bajeti ya mwaka
2015, inamruhusu Ofisa Masuhuli kuhamisha fedha kutoka kifungu kimoja
kwenda kingine, ili mradi asivuke asilimia saba ya bajeti nzima.
Kadhalika, kwa upande wa Waziri,
alisema sheria hiyo inampa uwezo wa kufanya uhamisho wa fedha kutoka
kifungu kimoja kwenda kingine ili mradi asizidi asilimia 10 ya bajeti na
katika uhamisho uliofanywa na wizara tajwa, mambo hayo yamezingatiwa
0 Response to "TUME YA MIPANGO YAMPA SOMO MBOWE JUU YA BAJETI"
Post a Comment