STAA OMMY DIMPOZ AMEAMUA KUINGIA KWENYE KILIMO BAADA YA GAME KUWA NGUMU By:chungwa.com. Posted: Monday 18th April 2016

blogger templates



12965888_222618848093998_1469943721_nZamani tuliamini kuwa kilimo hufanywa na watu wanaoishi vijijini tu. Mambo yamebadilika na kwasababu sasa hivi hakichukuliwi kama kilimo peke yake, bali biashara ya kilimo na leo vijana wengi wa mjini wamejiingiza huko sababu kinalipa.
Wakati ambapo unadhani kuwa Ommy Dimpoz yupo kimya kimuziki, basi anapenda kukufahamisha kuwa naye ni miongoni mwa vijana wa mjini walioingia kwenye biashara hiyo.Alipost picha Instagram akiwa kwenye shamba lake na kuweka emoji za matunda, ikiashiria kuwa huenda atafanya kilimo cha aina hiyo kwa sasa.Ni jambo zuri kwa vijana kuingia kwenye kilimo hasa kwakuwa tangu zamani inafahamika kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa na katika zile fursa 10 alizotaja Ruge Mutahaba, hiyo ni fursa ya kwanza. Heko Dimpoz.chanzo na Bongo5

0 Response to "STAA OMMY DIMPOZ AMEAMUA KUINGIA KWENYE KILIMO BAADA YA GAME KUWA NGUMU By:chungwa.com. Posted: Monday 18th April 2016 "

Post a Comment